Search This site

Thursday, November 11, 2010

DADA AGHADHABIKA KWA “SEHEMU” ZAKE KUGUSWA OVYO

Na Hosea K. Mburu

Kulitokea kizaazaa siku ya Jumanne baada ya kipusa mmoja kudai kupapaswa makalio na kalameni mmoja. Kisa hicho kilichotokea katika barabara ya kutoka maktabani kuelekea mabweni ya ‘L’ na ‘K’, kilivutia umati mdogo wa watu uliotaka kujua haswa kilichokuwa kikijiri!
Kisa hicho kilichotokea mwendo wa saa moja unusu jioni hivi, kilimkasirisha kidosho huyo kiasi cha kumvaa mzimamzima kalameni huyo na kutaka kupewa sababu halisi ya kuguswa sehemu hizo!”Wewe unacheza na mimi,unanijua lakini?Wewe ni nani kwangu hata ukanigusa!wewe shetani sana!shetaniiiiiii!”Alifoka mrembo huyo bila uwoga.Jamaa huyo aliyeonekana kuwa mlevi chakari hakugutushwa kamwe na malalamiko ya mwanadada huyo kwani alionyesha nia ya kutaka kumgusa dada huyo tena.
Juhudi za wapita njia kumrai dada huyo kumpuuzilia mbali jamaa huyo na kujiendea na hamsini zake, katu hazikuzaa matunda kwani alitishia kuripoti kisa hicho kwa walinzi.Hata hivyo, jamaa huyo aliyekuwa amepiga mtindi kupindukia alipuuza vitisho hivyo,”Kama ni security nenda uwaite, mii…. mi mii….. mi Joni, siogopi mtu, mimi naogopa Mungu na njaa peke yake,”jamaa alitamka kwa kejeli na kutojali!
Mrembo huyo alijaribu kumvuta jamaa huyo ili kumkabidhi mikononi mwa walinzi lakini aliambulia patupu kwani alizidiwa nguvu. Juhudi zake za kuomba msaada ili kukabiliana na jombi huyo hazikufua dafu kwani wapita njia waliwapuuzilia mbali! Wengine walisikika wakimlaumu dada huyo haswa kulingana na mavazi yake ya kubana na kuchochea aliyokuwa ameyavaa. Dada huyo baada ya kuona matarajio ya “mshenzi” huyo kurudiwa yakififia, hakuwa na budi ila kujiendea zake! Huku jamaa naye akatoweka marshimarshi.
Kisa hicho kiliibua suala nyeti kuhusu mavazi “yasiyoridhisha”, haswa miongoni mwa akina dada wenye mazoea ya kujivalia nguo zinazowabana kikiki kiasi cha maumbile yao kuonekana bayana. Waama ni hoja ya uhakika kuwa pengine mavazi hayo ya “NGUO SIKUVAA NA UCHI SIKUKAA” ndio huleta majaribu kwa kaka zetu kama jamaa huyo ambaye aliyepatwa na mshawasha na kulazimika kufanya mambo yatakayo wavunjia vipusa heshima na taadhima yao!Usisahau visa vya Mungiki na vikundi vinginevyo humu nchini vya kuwatoa nguo akina dada wasiovalia kiistaarabu!

WETANGULA HATIMAYE ASALIMU AMRI
Waziri wa mambo ya nje, Bw. Moses Wetangula, na katibu wake wa kudumu, Thuita Mwangi, hatimaye wamesalimu amri na kujiuzulu.Wawili hao wamejiuzulu kutokana na kashfa inayohusisha senti zaidi ya kima cha BILIONI MBILI za kugharamia jumba la ubalozi wa Kenya kule Tokyo,Ujapani.
Hata hivyo,bunge jana jioni likiongozwa na Waziri Mkuu lilipitisha mswada wa kamati ya bunge iliyotaka wawili hao kujiuzulu ili kutoa fursa maridhawa ya uchunguzi zaidi kuhusiana na kashfa hiyo.Waziri alisisitiza kwamba hana hatia na kuwashutumu mahasimu wake wa kisiasa kwa madhila yanayomkumba!
Tukio hili limetokea siku chache tu baada ya aliyekuwa Waziri wa elimu za ngazi za juu, Bw. William Ruto, kusimamishwa kazi kwa muda ili kuruhusu uchunguzi wa madai ya utapeli!
Wakenya mnaodai mu wazalendo, MPO???

0 comments:

Post a Comment